Habari

Serikali yatoa miezi 3 kwa NHC kukamilisha miradi yote ya ujenzi wa nyumba

Serikali imetoa miezi mitatu kwa shirika la nyumba la taifa NHC liwe limekamalisha miradi yote ya ujenzi wa nyumba zinazojengwa kwa ajili ya kuuzwa kwa wananchi kwa gharama nafuu hatua ambayo itatoa nafasi kwa serikali kupitia shirika hilo kuendelea na miradi mingine ya nyumba katika kupunguza tatizo la makazi hapa nchini.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, ametoa agizo hilo baada ya kutembelea nyumba 50 zinajengwa na shirika hilo eneo la Buhare katika manispaa ya Musoma, ambapo amesema kuwa kuchelewa kukamilika kwa miradi hiyo kwa wakati, kunachangia kuliingizia shirika hilo katika gharama kubwa za ujenzi wa nyumba hizo.

“Tangu 2014 mmeanza ujenzi wa nyumba hizi haziishi, lakini wangekuta hizi nyumba zimejengwa haraka zinaisha pengine wangepata matumaini, sasa unajua mtu akikupa nyumba hizi hajui zitaisha lini, sasa anakuwa ameona tangu imeanza kujengwa, mwaka wa kwanza unakatika, mwaka wa pili una katika, mwaka wa tatu, March nyumba hizi ziishe,” alisema Lukuvi.

Kwa upande wake meneja wa NHC mkoa wa Mara, Frank Mambo, amemueleza waziri huyo kuwa ujenzi wa nyumba hizo upo katika hatua za mwisho, huku akiwaomba wananchi na taasisi za serikali kujitokeza sasa kununua nyumba hizo za kisasa.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents