Habari

Serikali yatoa onyo kwa mawakala wa forodha wanaogushi nyaraka

Serikali kupitia Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Samwel Manyele imewapiga marufuku mawakala wa forodha wanaogushi nyaraka kwa ajili ya kuingiza kemikali kwani ni kinyume cha Sheria na pia wanaipotezea Serikali mapato.

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari, Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Prof. Samwel Manyele alipokuwa akizungumza kuhusu uingizaji wa kemikali nchini kutoka nje ya nchi.

“Natoa onyo kwa mawakala wote wa forodha wasiofuata taratibu zilizowekwa na Serikali hasa wanaogushi nyaraka zenye lengo la kukwepesha Sheria na kukwepa kulipa kodi na tozo mbalimbali za Serikali hivyo watakaokaidi hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao,” amesema Prof. Manyele.

Hata hivyo, Prof. Manyele amesisitiza kuwa kuanzia Leo Agosti 17,mwaka huu hakuna mtu atakayeruhusiwa kujishughulisha na shughuli za kemikali bila kuwa na hati ya usajili wa shughuli anayoifanya pia hakuna atakayeruhusiwa kuagiza mizigo ya kemikali bila kuwa na kibali.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents