Serikali yatoa sababu za kukatika kwa umeme Dar (+video)

Serikali kupitia Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Matogoro Kalemani imeeleza sababu zinazopelekea kukatika katika kwa umeme jiji la Dar es es salaam.

Dkt. Kalemani amesema kuwa kukatika kwa umeme kuna tokana na sababu nyingi, si kwa sababu ya kutokuwepo kwa umeme au miundombinu.

Kalemani ameyasema hayo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge Temeke (CUF), Mh. Abdallah Mtolea aliyetaka kujua sababu zinazopelekea kukatika kwa umeme jiji la Dar es Salaam hasa Temeke.

“Kukatika kwa umeme kuna tokana na sababu nyingi, si kwa sababu ya kutokuwepo kwa umeme au miundombinu. Wakati mwingine ni kasoro ndogo ndogo, tunakiri kabisa zipo changamoto za maeneo machache za kukatika kwa umeme kwenye baadhi ya nyakati za mida tutashirikiana na Wabunge kutatua matatizo hayo. Tunachokiomba ni kutupa taarifa inapotokea hitilafu ya namna hiyo,” amesema Kalemani.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW