Tupo Nawe

Serikali yawahakikishia umeme wa uhakika wananchi wa Mbagala

Serikali kupitia Naibu Waziri wa Nishati,Subira Hamisi Mgalu imesema kuwa hali ya umeme katika maeneo ya Mbagala umeimarika na imewahakikishia wakazi wa maeneo hayo kuwa hali ya umeme inaendelea kuwa ya uhakika.

Hayo yameelewa leo, Mei 16 Naibu Waziri, Subira wakati akijibu swali Mbunge wa Mbagala, Isa Ali Mangungu aliyehoji, Je? ni lini ujenzi wa kituo kidogo cha kupooza umeme Mbagala utakamilika?

“Ili kuimarisha hali ya upatikani wa umeme katika jiji la Dar es salaam hasa maeneo ya Mbagala shirika la Umeme (TANESCO) nchini mwezi Februari 2018 kupitia mradi wa TEDAP ilikamilisha njia za uboreshaji wa njia za usafirishaji, usambazaji na vituo vya kupooza umeme katika mikoa ya Dar es esalaam, Arusha na Kilimanjaro na mradi huu ulitekelezwa kwa ufadhili Benki ya Dunia, ” alisema Subira.

Aidha amesema Kukamilika kwa mradi huu kumeimarisha upatikanaji wa umeme katika eneo la Mbagala ikilinganishwa na kipindi cha nyuma.

Hata hivyo, serikali imesema kwasasa hali ya umeme umeimarika katika meneo ya Mbagala na wizara yake itaendelea kushirikiana na Mbunge na wananchi kuhakikisha hali ya umeme mbagala inaendelea kuwa ya uhakika.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW