Habari

Serikali yawataka wadaiwa sugu NSSF kulipa madeni yao

Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, sera, bunge, kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu, Jenista Muhagama, amewaagiza wadaiwa wote wa shirika la hifadhi ya jamii NSSF, kulipa madeni wanayodaiwa mara moja ili kufankisha mipango ya maendeleo ya shirika hilo.

jenista

Ametoa agizo hilo katika ziara yake fupi ya kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba wa Dungufam unaotekelezwa na NSSF uliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

“Tuchukue tu hatua haraka,tena kwa kuzingatia mikataba hiyo hiyo, kwasababu kila mtu alipokuja kukopa alijua mkataba wa ukopaji wake kati yake yeye na NSSF ukoje na unafanyaje na masharti yake yake ya kulipa yako vipi,” alisema.

“Ndani ya wiki moja, ninataka kuhakikisha mnachukua hatua haraka sana kushughulika na hao wadaiwa sugu bila kujali ni nani,anafanya nini katika nchi hii ya Tanzania na yuko wapi,” alisisitiza Mugahama.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents