Habari

Serikali yaweka mikakati kudhibiti haki za kazi za wasanii wa muziki na filamu

Waziri wa Habari, Utamaduni, na Michezo Dk Fenella Mukangala amesema serikali imewaka mikakati ya kudhibiti haki za kazi za wasanii wa muziki na filamu.

PIX2

Akijibu hoja ya kamati ya maendeleo ya jamii bungeni jana, Dk Fenella alisema nyimbo nyingi za wasanii zinazotumiwa katika vifaa vya mawasiliano vinaendelea kuwanyonya wasanii kutokana na mikataba waliyoingia wasanii.

“Kuna haja ya kukaa na wadau kuona kuna nini cha kufanya,” alisema Dk Fenella. “Hata hivyo serikali kupitia urasimishaji ambao tumekwisha uzungumza, imeaanda mikataba bora ambayo inayoonyesha bayana namna kazi za filamu ama muziki zitakavyotumiwa katika mifumo ya mawasiliano,itakayoomwezesha mhusika kupata haki yake stahiki. Basi tunaomba wale wanaohusika wahakikishe wanatumia hizi sheria na kuwasiliana na bodi ya filamu ili kazi zao ziwe katika hali nzuri.”

Pia alisema serikali imeanzisha utaratibu wa kubandika stempu za kodi katika bidhaa za filamu na kazi za muziki ili kubaini kazi halali na fake.

“Stamp hizo zinafanyika nje ya nchi hivyo siri za utengenezaji wake haziingii mikononi msimo salama. Nasema hivi kwasababu ilijitokeza wakati wa kuchangia zipo kazi ambazo zinazunguka na stamp bandia.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents