Habari

Serikali yazifungia shule 40 za msingi na sekondari zisizo na usajili

Wizara ya elimu, Sayansi,teknolojia na mafunzo ya ufundi imezifuta shule za awali, msingi na sekondari nchini zaidi ya 40 ambazo hazijasajiliwa.

img_5310-1280x853

Kaimu Mkurugenzi wa Usajili wa shule katika wizara hiyo, Khadija Mcheka, alisema Mei mwaka huu baada kuzipa miezi miwili shule ambazo hazijasajiliwa kufanya hivyo, walizifungia shule nyingine 12.

Shule zilizofungiwa kwa kuendesha shughuli zake bila usajili zilitajwa kuwa ni shule za awali na msingi za Must Lead ya mkoa wa Pwani, na za mkoa wa Dar es Salaam ni Brainstorm, Pax, Lassana, Grace, Rose Land, Julius Raymod, St Thomas, Mary Mother of Mercy, Noble Sinkonde, Immaculate Heart of Mary, St Columba, Corner stone, Dancraig, Mwalimu Edward Kalunga, Edson Mwidunda, Gisela, Kingstar, St Columba awali, Bilal Muslim, Thado, Hocet , Elishadai, Lawrance Citizen, Comrade, Dar Elite Preparatory na Golden Hill Academy na Hekima.

Nyingine ni Pwani Islamic, St Kizito na Rwazi Encysloped za Kagera, Dancraig na Qunu za Pwani, Hellen’s ya Njombe, Joseph ya Arusha, Samandito na Maguzu za Geita. Alizitaja shule za Sekondari zilizofungiwa kwa sababu hiyo kuwa ni Hananasif, Elu, Hocet, Safina za Dar es Salaam na Namnyaki ya Iringa.

“Baada ya kutoa tangazo kutokana na kubaini kuwapo shule nyingi zisizosajiliwa, wapo waliojitokeza na nyingine tumezifungia kutokana na kutokidhi viwango vya usajili lakini pia tunaamini wapo waliojificha wakiendelea kutoa huduma,” alisema Mcheka.

Aliwaagiza wakaguzi katika kanda na wilaya, kufanya ukaguzi na kutoa taarifa kwa zile ambazo hazijafungiwa na ikithibitika hazijasajiliwa, kuzifungia mara moja.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents