Habari

Serikali yazimwagia sifa shule za sekta binafsi

Seriali imezipongeza shule za sekta binafsi kwa ulipaji mzuri wa kodi na kutambua umuhimu wake katika kuleta maendeleo ya Taifa.

Akizungumza leo bungeni mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknojia, Ole Nasha amesema kuwa kwa kutambua ushirikiano ulipo na sekta binafsi imekuwa ikiondoa changamoto zinazowakabili wamiliki wa shule hizo kama kuondoa kodi na tozo mbalimbali.

“Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi kubora mazingira ya wao katika elimu tutendela kuboresha zaid ili wafanye kuwekeza kwa kiurahisi lakini vile vile naomba niseme kwamba sekta binafsi wamekuwa walipaji wazuri wa kodi na wanatambua umuhimu wa kulipa kodi katika maendeleo ya Taifa kwa hiyo na kwamba tupo pamoja katika kukabiliana nao kuhusiana na namba ya kuweza kuangalia namna ya kupunguza hizo kodi bado tunasisitiza kwamba ni vizuri tukaendelea kushirikiana ili kuhakikishia baadhi ya gharama ambazo ni mhimu ziweze kulipwa na wale ambao wanaweza kuchangia,” amesema Nasha.

Hata hivyo, Serikali imesema inatambua umuhimu wa sekta binafsi katika utoaji wa elimu, ili kuakikisha mazingira rafiki katika utoaji wa elimu serikali imekuwa ikifanya majadiliano na sekta binafsi kwa lengo la kuondoa changamoto zinazo wakabili hadi sasa serikali imeweza kuondoa kodi na tozo mbalimbali ambazo awali walikuwa wakitozwa wamiliki wa shule binafsi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents