Habari

Serikali yazungumza kuhusu masalia ya Mijusi nje ya nchi

Wazo la kuwarudisha nchini Dinosaria halina tija kutokana na ugumu wa Kiteknolojia na gharama ikilinganishwa na faida za kuchukua hatua hiyo.

 

Akijibu swali la Mbunge wa Mchinga Mhe. Hamidu Hassan Bobali lililo uliza,Ni nini kauli ya mwisho ya Serikali kuhusu faida ambayo wananchi wa Lindi na Tanzania kwa ujumla wananufaika kutokana na mabaki hayo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Ramo Makani amesema Tanzania itaendelea kusisitiza kupata manufaa kutokana na uwepo wa Dinosaria wake huko Berlin-Ujererumani.

“Kufuatia majadiliano ya kina yaliyohusisha wataalamu wabobezi katika masuala ya Malikale kutoka pande zote mbili imekubalika kuwa Serikali ya Ujerumani itaendesha shughuli za utafiti zaidi huko Tendaguru na katika maeneo jirani ili kuwezesha uchimbaji wa mabaki ya Dinosaria wengine yanayoaminika kuwepo katika maeneo hayo pamoja na kuanzisha Kituo cha Makumbusho ili shughuli za Utalii zifanyike katika eneo hilo na kuvutia watalii kutoka nchini na nje ya nchi” alisisitiza Mhe. Makani.

Kuhusu Serikali kupunjwa mapato yatokanayo na viingilio katika Makumbusho ya Elimu Viumbe ya Berlin,Mhandisi Makani amesema jambo hilo halina ukweli wowote kwani ni ngumu kufahamu ni kiasi gani hupatikana kama kiingilio kuwaona Mijusi kutoka Tanzania kwakuwa Makumbusho hiyo ina kumbi nyingi zenye masalia kutoka nchi mbali mbali za Afrika na gharama za kuendesha Makumbusho hiyo hutolewa na Serikali ya Ujerumani.

Ameeleza kuwa Serikali ya Ujerumani itafadhili zoezi la uimarishaji idara inayohusika na Malikale katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuwezesha upatikanaji wa wataalamu wa kutosha wa fani husika ilikuendeleza Utalii wa Malikale nchini.

Mijusi mikubwa (Dinosaria) ilichimbwa katika Kilima cha Tendaguru,mkoani Lindi kati ya waka 1909 na mwaka 1913 na kupelekwa katika makumbusho ya Elimu Viumbe ya Berlin nchini Ujerumani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents