Michezo

Sevilla yatinga fainali ya Copa del Rey kibabe

Klabu ya Sevilla usiku wa kuamkia leo imefanikiwa kutinga fainali ya kombe la Mfalme nchini Hispania kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Leganes.

Kwenye mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya goli 1-1 ambapo Sevilla imetinga fainali kwa jumla ya magoli 3-1.

Magoli hayo yaliyofungwa na Joaquin Correa na Franco Vazquez yamekamilisha safari ya Secvilla ambapo leo kuna mtanange mwingine kati ya Barcelona na Valencia ili kupata timu nyingine ya kwenda fainali.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents