Burudani

Sex Tour kumpeleka Idris Sultan kwenye jukwaa la wachekeshaji Afrika Kusini (Picha)

Mchekeshaji Idris Sultan amealikwa kuhudhuria tamasha kubwa la Komedi litakalofanyika mwezi huu nchini Afrika kusini lililoandaliwa na Comedy Central , moja kati ya taasisi kubwa Duniani katika tasnia ya ucheshi na uchekeshaji.

Mchekeshaji Idris sultan akiburudisha maelfu ya wakazi wa Dar es salaam na viunga vyake waliofika katika tamasha la Komedi maarufu kama SEX TOUR hivi karibuni katika ukumbi wa Club next door Arena Jijini Dar es salaam.

Mualiko wa Idris unakuja baada ya msanii huyo wa tasnia ya uchekeshaji kufanya Tamasha la Sex Tour ambalo liliwavuta maelfu ya wapenzi wa comedy hapa nchini .

Kwa mujibu wake mualiko wa huo ni sifa kubwa kwa Taifa, baada ya bongo flava kutoboa kimataifa, sasa ni zamu ya tasnia ya uchekeshaji wa Tanzania.

Idris akiwa anapima afya yake katika madhimisho ya siku ya ukimwi duniani huku akiongozana na wachekeshaji wenzake kuhamasisha vijana kutokuwa na woga wa kupima na kujua hali zao.

Akizungumzia kuhusu tamasha la Sex Tour Idris alisema lilikuwa na lengo kuu ya kuburudisha na kuelimisha watu katika ma swala mbali mbali ya kijamii kwa kutumia Sanaa ya uchekeshaji.

“Tarehe 1 December Idris Sultan aliandaa tamasha la kwanza la Sex Tour katika ukumbi wa Next Door Arena. Watu zaidi ya 7,000 walihudhuria huku wengi wakilalamika kukosa ticket.

Jaymondy akiwavunja mbavu maelfu ya watazamaji waliojitokeza katika ukumbi wa Club next door katika Tamasha la Komedi maarufu kama Sex Tour liliofanyika hivi karibuni hapa jijni Dar es salaam.

SexTour imekua tamasha kubwa zaidi la comedy kuwahi kutokea nchini Tanzania na kufananishwa na baadhi ya matamasha makubwa ya muziki” anasema

Likibeba ujumbe “Kutokupima hakubadili matokeo”tamasha hilo lilihudhuriwa na wachekeshaji mbali mbali akiwemo Jaymondy, Mkaliwenu, Dogo pepe, Coy Mzungu, Blackpass,kitenge,Nalimi ,Optalema Deo, Max, Young Unstopable ,D comic na wengine wengi huku upande ma muziki wa kizazi kipya ukiwalishwa vyema naa Whozu na Billnass.

“Changamoto za maambukizi mapya kwa vijana wa umri 15-24 bado ni kubwa, hivyo Sex Tour ilikua inalenga zaidi kushauri vijana kujali afya zao, kutokuwa na hofu ya kupima afya zao lakini pia kubadili fikra potovu za kuwa nyanyapaa wenye maambukizi,”anasema Idris.

Idris sultan akiendelea kuvunja mbavu za maelfu za wakazi wa Jiji la Dar es salaam katika jukwaa la Club next door Arena katika Tamasha la komedi maarufu kama Sex Tour liliofanyika hivi karibuni Jijini Dar es salaam.

Tamash la Sex Tour lilidhaminiwa na Mfuko wa dharura wa Raisi wa Marekani wa kupambana na maambukizi ya Ukimwi (PEPFAR) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents