Uncategorized

SGA yapongezwa kwa kukuza teknolojia nchini Tanzania

Kampuni ya SGA Tanzania ambayo inajishughulisha na utoaji wa huduma kwenye sekta ya ulinzi imepongezwa kwa kukuza teknolojia, baada ya kuibuka mshindi wa tatu wa jumla kwenye maonyesho ya kimataifa ya teknolojia ya madini (International Mining Technology Exhibition) iliyomalizika hivi karibuni mjini Geita.

Mkurugenzi Mtendaji wa SGA Tanzania Eric Sambu akipokea tuzo kutoka kwa meneja mauzo na masoko wa kampuni hiyo Faustine Shoo.

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Mh. Angela Kairuki, ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi kwenye maonyesho hayo, aliipongeza kampuni hiyo kwa kuingiza teknolojia za kisasa hasa kwenye sekta ya madini.

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Mh. Angela Kairuki akikabidhi tuzo kwa Meneja Mauzo na Masoko wa SGA Tanzania Faustina Shoo wakati wa sherehe za ufungaji wa maonesho ya kimataifa
Maonyesho hayo pia yalishirikisha washiriki mbalimbali kutoka Tanzania na nje ya nchi.

Waziri Kairuki alisema SGA Tanzania pia imesaidia kutoa elimu kuhusu teknolojia za kisasa, zinazosaidia kwenye utoaji wa huduma za ulinzi hapa nchini.

Akizungumza wakati wa upokeaji wa tuzo hizo, meneja wa mauzo na masoko wa SGA Tanzania Faustine Shoo, alisema tuzo hiyo ni ishara kuthibitisha ubora za huduma zinazotolewa hasa kwenye uwekezaji wa teknolojia uliofanywa na kampuni hiyo katika kipindi chote tangu kuanzishwa kwake.

Baadhi ya wafanyakazi wa SGA Tanzania walioshiriki maonesho hayo wakiwa katika banda la kampuni hiyo.

“Tumeweza kuthibitisha namna teknolojia mpya za ulinzi zinaweza kusaidia kuboresha ulinzi kwenye maeneo ya migodi na kupunguza uwezekano wa kupata hasara. Kwa teknolojia hizi, migodi ya madini itakuwa sehemu salama kwa ajili ya kufanya kazi na serikali itafikia kusidio lake la kuthibiti bidhaa za madini kwaa ajili ya maendeleo ya uchumi,” alisema.

Alisema kuwa SGA Tanzania inafanya kazi na kampuni kubwa za madini hapa nchini na faida zake zimeonekana kwani migodi mingi imedhibiti shighuli zake na kuimarisha ulinzi.

Naye Mkurugenzi wa SGA Tanzania Eric Sambu alisema amefurahishwa na kutambuliwa kwa kampuni yake katika utoaji wa huduma bora, na hii imethibitisha kwamba wanaweza.

Aliwapongeza wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa kuonyesha uwezo wake masuala ya ukuzaji wa teknolojia na kuhakikisha thamani ya fedha za wateja.

Alisema ulinzi ni suala muhimu kwenye uwekezaji katika sekta ya madini kwani inaongeza tija na SGA Tanzania inajivunia kwa kushiriki kutimiza hayo.

“SGA Tanzania ni kampuni ya kwanza binafsi kutoa huduma za ulinzi hapa Tanzania na imeonyesha umahiri wake kutokana na kuwa na timu yenye motisha,” alisema.

“Kwa timu ya wafanyakazi 18,000 kwenye kampuni, iliyoanzishwa miaka 50 iliyopita dhima na dira yetu ni watu. Tumewekeza zaidi kwenye mafunzo na tunahakikisha kwamba tunalipa zaidi ya viwango vya soko kuwapa motisha na kuhakikisha hawahami,” aliongeza.

Alisema wakati kampuni inaadhimisha miaka 36 ya uwepo wake nchini Tanzania, kumekuwepo na ukuaji, hasa kipindi cha miaka mitano iliyopita kutokana na mapinduzi na shughuli ambazo zimekidhi mataraji ya wateja.

Mkurugenzi huyo alisema kwamba mafanikio waliyoyapata ni jitihada za wafanyakazi ambao wanafanya kazi kwa moyo, huku kukiwa na ufuatiliaji wa utimizaji malengo ya mkampuni.

“Yanayotokea kwenye biashara za ndani yametufunza na kutupa nafasi ya kupata fursa ya kuwawezesha wafanyakazi wetu kufanyakazi kuendana matarajio ya wateja,´alisema

Alisema uboreshaji wa muenendo wa shughuli za kibiashara, uwekezaji kwenye teknolojia na mafunzo ya wafanyakazi yameiwezesha kampuni kuwa na muelekeo mzuri.

Sambu alisema kampuni hiyo imeendelea kutimiza masuala ya viwango vya kimataifa, hasa cheti cha ISO kwenye mifumo ya ufanyaji kazi tangu mwaka 2001 na hivi karibuni imepata cheti za ubora wa kimataifa wa afya na usalama kazini kazini (Occupational Health and Safety ISO 45001 Standard” na pia kupata cheti cha ISO 18788 kwenye masuala ya ulinzi (Security Management Operations System) na kuwa ya kwanza Tanzania.

SGA ni kampuni kongwe ya ulinzi Tanzania iliyoanzishwa mwaka 1984 ikijulikana kama Group Four na imeajiri watanzania takribani 6,000.

Mwisho

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents