Shaa: Nipo kwenye uchunguzi kujua aliyeivujisha ‘Baba Kodi’

Jana tuliweka wimbo mpya wa Shaa uitwao Baba Kodi na kuuchambua kidogo jinsi ulivyo na ujumbe muhimu kwa wamiliki wa nyumba na wapangishaji mjini. Hata hivyo imebainika kuwa Shaa hakuachia wimbo huo na bado anaendelea kuchunguza ili abaini nani aliyeuvujisha.

AUDIO: SHAA ASEMA NA BABA WENYE NYUMBA ‘WANOKO’ KWENYE BABA KODI

shaaaa

Akiiambia Bongo5 kupitia Twitter, Shaa amesema, “thank u 4 the love…however huo wimbo #BabaKodi umetolewa bila my consent..nipo ktk pirika za kuchunguza who leaked it.”

Ni hivi karibuni tu Shaa aliachia wimbo wake mpya uitwao Promise pamoja na video yake na pia ameshashoot video nyingine ya wimbo uitwao Lava Lava huku muongozaji akiwa Adama Juma wa Visual Lab: Next Level.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents