Michezo

Shaban Nditi anena mazito Mtibwa kupoteza kwa mara ya kwanza VPL

Mtibwa Sugar hapo jana walipoteza mchezo wao wa kwanza katika ligi kuu bara (Vodacom Premier League)  tangu msimu wa 2017/2018 uanze.

Shaban Nditi wa Mtibwa Sugar (kushoto) na  George Kavila wa Kagera Sugar (kulia) wakiongea na waamuzi

Mtibwa Sugar walipoteza mchezo wa jana dhidi ya Kagera Sugar kwa goli 1-0, goli hilo  lilipatikana kwa mkwaju wa penalty katika dakika ya 82 likifungwa na Edward Christopher baada ya Dickson Daud kuunawa mpira katika harakati za kuokoa.

Baada ya mchezo huo mtandao klabu www.mtibwasugar.co.tz umezungumza na nahodha wana tam tam, Shaban Mussa Nditi ili kupata machache juu ya mchezo  huo dhidi Kagera Sugar.

“Tumepoteza tulipigana lakini wenzetu wamefanikiwa kupata penati na kuitumia na kushinda, makosa yaliyotokea na kupelekea sisi kupoteza mwalimu kayaona na atayafanyia kazi na mashabiki wa Mtibwa Sugar hawapaswi kukata tamaa ligi bado mbichi na waje watupe Support katika mchezo ujao dhidi ya Azam ”  Nditi

Wana tam tam wanabaki katika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi baada ya matokeo hayo ya jana na mchezo ujao wana tam tam wanataraji kusafiri hadi jijini Dar es laam kuwakabili Azam.

Mchezo namba 88  dhidi  ya Azam unatarajiwa kuchezwa Jumatatu ya tarehe November 27 katika uwanja wa Chamazi Complex.

Kikosi kilichocheza dhidi ya Kagera

Benedector Tinocco, Rodgrs Gabriel “Jigwa” , Issa Rashid “Baba Ubaya’, Cassian Ponera ‘Pepe’ , Dickson Daud Mbeikya, Shaban Mussa Nditi, Saleh Khamis Abdallah, Hassan Dilunga, Kelvin Sabato, Stamil Mbonde/Riphat Khamis, Haruna Chanongo/Ismail Aidan

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents