Habari

Shabiki amtishia J.Cole asipo retweet ujumbe wake atampiga risasi mdogo wake mwenyewe!!

Rapper J.cole jana (June 18) ameachia rasmi album yake mpya ya ‘Born Sinner’ lakini masaa machache kabla album hiyo haijatoka shabiki mmoja alimuandikia ujumbe twitter na kumtaka a-retweet vinginevyo angempiga risasi mdogo wake mwenyewe.

J.Cole twitter
Jumatatu (June 17) usiku shabiki huyo ambaye haikufahamika anatokea wapi aliandika tweet hiyo iliyoambatana na picha ya msichana mdogo akiwa ameelekezewa bastola kichwani kwake, na kumtaka J.Cole a retweet ili aweze kununua album yake ‘Born Sinner’ na akishindwa kufanya hivyo atampiga risasi mdogo wake wa kike.

Mtu huyo alitweet “@JColeNC retweet me and I’ll buy Born Sinner. Don’t retweet me and I’ll kill my lil sister.”

Baada ya tweet hiyo muda mfupi baadaye rapper huyo alifanya kile alichokihitaji shabiki huyo kwa ku retweet ujumbe huo uliokuwa umeambatana na picha ya msichana mdogo aliyeelekezewa bastola kichwani.

Jumanne asubuhi (June 18) Rapper Cole alitweet ujumbe mwingine kuhusiana na tukio hilo “Wildest s**t I ever seen on twitter.”

Mtandao wa TMZ ulijaribu kuwasiliana na idara ya polisi ya Carolina kaskazini, Marekani anakotokea J.Cole lakini hawakuwa na taarifa zozote kuhusiana na swala hilo.

Masaa machache baadaye shabiki huyo alikuja kutweet akidai bastola iliyoonekana kwenye picha ile ni BB GUN na kudai kuwa mtoto huyo hakuwa katika hatari yoyote.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents