Michezo

Shabiki mkereketwa wa Yanga, Steve apata zali la kwenda SuperSport Afrika Kusini

Baada ya kupata umaarufu wa faida kupitia ushabiki wake kwa timu ya Yanga, shabiki maarufu wa timu hiyo, Yanga, Steven Samwel amepata mwaliko wa kwenda kufanyiwa mahojiano na kituo maarufu duniani kwa kurusha matangazo ya mpira, Super Sport.

IMG_1721
(Kulia)Shabiki wa Yanga Steven akimlaki Okwi wakati akitua jangwani

Akizungumza na BBC, Steven, amesema baada ya SuperSport kupata clip ya video yake walimpa mwaliko wa kwenda Afrika Kusini kufanya nao mahojiano.

“Nimepata mialiko mingi sana, walikuja The Citizen,na wewe mwenyewe BBC umekuja hapa umenifuata mimi,umetoka kule mbali mpaka kunifuata mimi na hivi ninavyoongea hapa mwandishi wa habari nimepata zali hapa la kwenda SuperSport mwezi wa nne nashuka bondeni South Africa kutokana kwamba South Africa walipata clip Yangu baada ya kufungwa goli tano kwa bila na Simba wakasema huyo mtu haiwezekani tupate clip yake tu inabidi tumwalike moja kwa moja kuja South Africa ili tufanye naye mahojiano,” alisema Steve.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents