Michezo

Shabiki namba moja wa Yanga SC afariki dunia

Mwanachama aliejizoelea umaarufu mkubwa ndani ya klabu ya soka ya Yanga SC  na nchini kwa ujumla aliyefahamika kwa jina maarufu la Ali Yanga amefariki dunia.

Mwanachama wa klabu ya Yanga SC aliyefahamika kwa jinala Ally Yanga enziza uhai wake

Kwa mujibu wa  mtandao wa Twitter wa timu hiyo umeeleza kuwa mwanachama huyo amefariki dunia kwa ajali ya gari leo hii alipokuwa katika mbio za Mwenge.

Katika taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imesema kifo cha shabiki huyo kimeacha pengo kubwa kwa nafasi yake ambayo ilipelekea kujipatia umaarufu mkubwa pamoja na kuwa balozi mzuri kama mwananchama wa timu hiyo.
Marehemu atakumbukwa kutokana na mbwembwe zake alizokuwa akizionesha anapokuwa uwanjani na nje ya uwanja hasa pale timu yake inapokuwa katika mchezo. Bongo5 tunatoa pole kutokana na msiba huo

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents