Tupo Nawe

Shabiki wa Simba aliyetembea kwa miguu umbali wa zaidi ya Km 820 kutoka Mbeya kuja Dar, awakuna TP Mazembe washindwa kujizuia na kutoa ya moyoni

TP Mazembe wameoneshwa kuguswa sana na Shabiki kindakindaki wa Simba aliyetemebea umbali wa kilometa 829.50
Shabiki huyo alianza safari yake kutoka Mbeya umbali wa siku 7 (alianza safari yake tarehe 26-3,) ili kuifuata mechi ya kihistoria kati ya miamba ya soka hapa nchini Simba Sports Club na Vigogo wa soka barani Afrika TP Mazembe.


Klabu hiyo TP Mazembe imemwagia sifa kemkem shabiki huyo ajulikanae kama Ramadhani Mohammed mwenye umri wa miaka 29 mkazi wa mbeya. Hii imetoa funzo kwao na kuweka heshima miongoni mwa mashabiki wa Simba na soka kwa ujumla hapa nchini.


Katika ukurasa wao wa Instagram, klabu ya TP Mazembe imesema ni heshima iliyotukuka kwa shabiki aliyejitolea kuvumilia jua na mvua na kuifuata klabu yake ili kujumuika na wana msimbazi wote.
Klabu hiyo imetoa rai pia kwa mashabiki wake hasa hasa wa nchini Congo, jiji la Lubumbashi na maeneo ya karibu kuwa wanatakiwa kuiga mfano wa Shabiki huyu mwenye uchungu na timu yake.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW