Burudani

Shaka za baadhi ya wabongo kuhusu ushindi wa Lulu AMVCA ni ushahidi kuwa kutojiamini ni tatizo la kitaifa

Maisha yanafurahisha sana wakati mwingine. Na kwakweli vitu vidogo vidogo vinavyochekesha na kushangaza, huifanya dunia isiwe sehemu inayoboa.

12826235_939780536129321_1574191582_n

Unajua kwa mfano mtu ukishazoea kushindwa, automatically akili yako inajitengenezea imani kuwa wewe ulizaliwa kushindwa tu. Ni mbaya zaidi imani hiyo ikitoka kwenye hatua binafsi na kuingia kwenye hatua ya kitaifa.

Kushindwa kwetu kwenye michezo ya kimataifa kwa mfano, kumewafanya watanzania wengi wajiaminishe kuwa Tanzania ni wa kushindwa siku zote. Tumejikatia tamaa na kuikubali hali hiyo. Tumejiaminisha kuwa sisi ni wa hivyo hivyo kiasi ambacho ikitokea mtu au kundi limefanya tofauti, inakuwa ngumu kuamini.

Nimesikitika sana baadhi ya watanzania wanaoushuku ushindi wa Elizabeth ‘Lulu’ Michael kwenye tuzo za AMVCA 2016 zilizofanyika Lagos, Nigeria. Mbaya zaidi ni pale ambapo wapo wanaoaminishwa kuwa ushindi wa Lulu umetokana na nguvu za giza. Yes, huenda bado hujasikia, lakini uvumi huo upo umeandikwa Instagram:

lulu-12

Inasikitisha kumtishwa msichana huyo skendo kubwa kama hii. Japo ujumbe wake umefutwa tayari, Lulu ameonekana kuumizwa na kuamua kusema yake:

Lulu-11

Katika kipindi ambacho watanzania wote tunapaswa kumpongeza na kumpaka kama tulivyofanya kwa kumuandalia mapokezi ya kishujaa ambayo yamewashtua hadi Afrika Magharibi, wapo watu wachache wanaojaribu kumkatisha tamaa. Kwanini watanzania tujichukulie poa hivi?

Leo hii imefika hatua kwamba tasnia ya muziki Tanzania ni ya tatu kwa ukubwa Afrika, baada ya Nigeria na Afrika Kusini. Tunaweza kupata umaarufu huo kwenye filamu pia. Waigizaji kama Lulu, Wema na wengine wenye uelewa mzuri wa lugha iliyokuja kwa meli (kimombo), wanaweza kuitangaza Tanzania kama wakiandaliwa mazingira mazuri.

Na siku zote biashara ya showbiz hufanikiwa kutokana na support inayopewa na mashabiki. Support hiyo hiyo ndiyo iliyompa ushindi Lulu kwakuwa mashabiki wake na wengine wenye uzalendo na nchi yao walimpigia kura. Kura ndizo zilizompa ushindi Lulu na sio uchawi! Sasa hizi shaka zinatoka wapi? Tujiamini watanzania wenzangu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents