Habari

Shambulio la bomu kwenye mabasi laua watu 126 Syria

Watu 126 wamepoteza maisha kufuatia shambulio la bomu kwenye mabasi yaliyokuwa yamebeba raia wanaokimbia machafuko katika miji ya Syria.

Msafara wa mabasi hayo ulishambuliwa Jumamosi. Watu 109 kati ya waliouwa walikuwa wanakimbia vijiji vya Al-Fu’ah na Kafraya wakati wengine walikuwa wafanyakazi wa misaada na waasi waliokuwa wakiulinda msafara.

Tabriban watoto 68 ni miongoni mwa waliouawa. Msafara wa mabasi hayo yaliyokuwa yameegeshwa muda huo, ulikuwa umebeba maelfu ya watu kutoka kwenye mji unaoshikiliwa na serikali na kuvamiwa na waasi huko kaskazini magharibi mwa Syria.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents