Habari

Shambulio la kigaidi nchini Burkina Faso limeua watu 14 wakati wakifanya ibada kanisani

Shambulio la kigaidi nchini Burkina Faso limeua watu 14 wakati wakifanya ibada kanisani

Watu karinbu 14 wameuwawa baada ya shambulio la wazi ndani ya kanisa nchini Burkina Faso. Waathirika wa shambulio hilo walikuwa wamehudhuria ibada katika kanisa la Hantoukoura, mashariki mwa nchi hiyo siku ya jumapili.

Watu waliokuwa wanafyatua risasi hizo bado hawajafahamika na hata lengo lao bado halijawekwa wazi.

Mamia ya watu wameuwawa katika taifa hilo katika miaka ya hivi karibuni zaidi na kundi la kigaidi la jihadist, kutokana na mvutano wa kikabila na kidini haswa katika mpaka wa Mali.

Taarifa kutoka serikalini zinasema kuwa watu wengi wamejeruhiwa.

Idara ya usalama imeitaarifu chombo cha habari cha AFP kuwa watu wenye silaha ndio wamefanya shambulio hilo, “wameteketeza waamini wakiwa pamoja na wachungaji na watoto”.

Chanzo kingine cha habari kimesema kuwa wanaume hao wenye silaha walitumia pikipiki.

Mwezi Oktoba, watu 15 waliuwawa na wawili walijeruhiwa vibaya katika shambulio lililotokea katika msikiti.

Mashambulio ya kigaidi yameongezeka nchini Burkina Faso tangu mwaka 2015, na kusababisha maelfu ya shule kufungwa.

Mgogoro kati ya nchi hiyo na nchi jirani ya Mali ,eneo ambalo wanamgambo wa kiislamu wamechukua eneo la kaskazini la nchi hiypo tangu mwaka 2012 kabla ya jeshi la Ufaransa kuwaondoa.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents