Bongo Movie

Shamsa na Gabo kuja na mpya baada ya ‘Bado Natafuta’

Wakali wawili ndani ya tasnia ya filamu, Shamsa Ford na Gabo Zigamba  baada ya kufanya vizuri na filamu ya ‘Bado Natafuta’, wanatarajia kuachia filamu yao mpya hivi karibuni.

Akiongea na Bongo5 Alhamisi hii, Shamsa Ford amedai kazi hiyo tayari imekamilika na kinachosubiriwa ni kuingia sokoni.

“Mimi na Gabo tukikutana kwenye filamu tunafanya vitu vikubwa sana, ukiangalia filamu ya ‘Bado Natafuta’ ni filamu kubwa ambayo imenipa mafanikio mengi. Kwahiyo mimi sina mengi yakusema juu ya ujio wetu mpya zaidi ya kusema ni kazi nzuri ambayo hapaswi mtu kuikosa,” alisema Shamsa.

Muigizaji huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwae Terry, amewataka mashabiki wa filamu zake kuendelea kumsupport katika kazi zake za filamu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents