Habari

Shangwe za Fiesta 2007-Mwanza

Fiesta Boda 2 BodaSafari ya Fiesta 2007 Shangwe Boda 2 Boda inajikita katika jiji la Mwanza ambapo mashabiki kibao wa jiji hilo wamejiandaa na kukaa mkao wa kishangwe shangwe na maandalizi kibao yamekwishafanyika

Fiesta Boda 2 Boda


Safari ya Fiesta 2007 Shangwe Boda 2 Boda inajikita katika jiji la Mwanza ambapo mashabiki kibao wa jiji hilo wamejiandaa na kukaa mkao wa kishangwe shangwe na maandalizi kibao yamekwishafanyika ili kuadhimisha utamaduni huo ambao huadhimishwa na wapenzi wa burudani na watanzania kwa ujumla kila mwaka.


Katika kuadhimisha shangwe hizo timu maalum imeshatua jijini humo tayari kwa kuweka mambo sawa ikiwa ni pamoja kuandaa makazi ya wasanii ambao watatua kwa kishindo cha ajabu jijini humo tayari kwa kufanya makamuzi.


Kama kawaida ya kampuni ya Prime Time Promotion ambayo ndio waandaaji wa tamasha hilo miaka yote, wameshakamilisha taratibu za ujio wa msanii Koffie ambaye anatarajiwa kukamua maonesho mawili katika ukumbi ya Yatch Club na uwanja wa CCM kirumba.


“lengo langu la kuja jijini mwanza ni kwa ajili ya kuweka mambo sawa kidogo kwani mimi ni mmoja kati ya ma dj ambao watakuwa mbele kabisa katika kuongoza show hizo za Fiesta 2007 shangwe boda to boda, nachosema wakazi wa mwanza wakisikia shangwe wajue wanaume ndio tunaingia” alisema Dj Mully Bling Bling ambaye hivi sasa yuko jijini humo kwa maandalizi zaidi.


Habari ambazo zimetufikia kutoka jijini mwanza ni wakazi wana shauku sana kuona jinsi jukwaa litakavyoshambuliwa na vijana kutoka kiumeni yaani TMK Wanaume na TMK Wanaume halisi, pamoja na wasanii kama Alikiba, Marlow, TID, Q-chief, K-Lynn, Jay Moe, Z-Anton, Chidi Benz na wengine kibao.


Tamasha hili ambalo limedhaminiwa na Kampuni ya Straight Music, linatarajiwa kuanzia jijini mwanza tarehe 10 ndani ya ukumbi wa Yatch Club na katika uwanja wa CCM Kirumbe mwezi huu na kufuatiwa na onesho la Bongo D’Salaam katika viwanja vya Leaders club maeneo ya Kinondoni.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents