Habari

Shangwe za kusherehekea Kombe la Dunia zaua na kujeruhi maelfu ya watu Ufaransa (+picha)

Shangwe za kusherehekea Kombe la Dunia zaua na kujeruhi maelfu ya watu Ufaransa (+picha)

Kukiwa na furaha kwa taifa la Ufaransa kutwaa Kombe la Dunia nchini Urusi hapo jana usiku, sherehe za kufurahia ubingwa huo zimeleta maafa nchini Ufaransa.

Maelfu ya watu wakishangilia ushindi wa Kombe la Dunia mjini Paris jana jioni (Picha na AP)

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail limeripoti kuwa mpaka asubuhi ya leo watu wawili wameshafariki dunia kwenye mlundikano na maandamano makubwa yaliyofanyika mjini Paris katika viwanja vya Champs Élysées.

Taarifa zimeeleza kuwa chanzo cha vurugu na mkanyagano ni Polisi mjini Paris, Nancy na Lyon waliokuwa wanatumia mabomu ya machozi na maji ya washawasha kuwatawanya watu waliokuwa wanashangilia mabarabarani kitendo.

Shirika la Habari la France 24 limeeleza kuwa zaidi ya watu milioni moja walikusanyika katika viunga vya jiji la Paris kuuzunguuka mnara wa Eiffel.

Polisi mjini Nancy imeripotiwa kuwa inawashikilia watu 30 ambao nao usiku wa jana mjini humo walikuwa wanapasua chupa za mvinyo na Whisky kwenye kingo za barabara.

Hata hivyo hakuna ripoti kamili ya watu waliojeruhiwa lakini inakadiriwa kuwa zaidi ya watu 3000 waliumizwa katika miji tofauti tofauti wengi wakiwemo watoto na wanawake.

Katika mji wa Lyon magari matano yamechomwa moto hiyo jana huku vurugu zikitokea kwenye baadhi ya maeneo mjini humo. Tazama picha za matukio mbalimbali za jana usiku

Jijini Paris watu wakishangilia ushindi wa Kombe la Dunia.
Watu wakifuatilia mpira Live kwenye screen kubwa katika viunga vya mnara wa Eiffel
Polisi wakitimiza majukumu yao mjini Paris
Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron akishangilia moja ya goli jana jioni mjini Moscow kwenye mchezo dhidi ya Croatia.
Baadhi ya watu wakitiwa mikononi mwa polisi kwa kuleta vurugu mjini Nancy.
Majeruhi
Polisi wakiwatawanya watu kwa maji ya washa washa.

Picha zote kwa hisani ya Mtandao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents