Michezo

Shaquille O’Neal aomba kazi ya upolisi katika jimbo la Florida

Mchezaji mstaafu wa mpira wa kikapu katika ligi ya NBA nchini Marekani, Shaquille O’Neal ameomba kuwa afisa wa polisi wa ziada kwenye mji wa Doral, Florida nchini Marekani.

Celebrities Visit SiriusXM Studios - August 11, 2014

O’Neal, mwenye urefu wa 7 ft. 1 anatarajia kufanya mtihani maalum kabla ya kujiunga na polisi wa mji huo uliopo maili 13 magharibi wa mwa jiji la Miami. Msemaji wa jiji hilo Christina Baguer ameliambia gazeti la Miami Herald kuwa mitihani hiyo itahusisha afya yake ya mwili na kisaikolojia.

Mchezaji huyo mwenye miaka 42 aliyewahi kuzichezea timu za Miami Heat, Boston Celtics na L.A. Lakers na zingine amewahi kuupita mtihani huo kabla.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents