Burudani

Sharon wa TPF 5 asimulia maswahibu yaliyowahi kumpata


Mshiriki wa shindano la Tusker Project Fame msimu wa tano kutoka nchini Uganda, Sharon ana mambo mazito ya kuumiza nyuma ya sauti yake tamu.
Mrembo huyo mwenye miaka 20 na kitu, alizungumzia kuhusu mateso aliyoyapata enzi akiwa mtoto kutokana na ukatili wa baba yake.
“Baba yetu alikuwa anaweza kutupiga kwa masaa kwa kosa dogo tu. Hakuwa tu mkali bali mlevi pia. Alimfukuza mama yetu na tukabaki wenyewe kuishi naye,” Sharon aliliambia gazeti la The Star la Kenya.
“Maisha yakawa magumu kwasababu tuliacha kwenda shule na mbaya zaidi alituacha. Mama aliyekuwa amerudi kwa wazazi wake aliamua kutuchukua japo hakuwa na uwezo wa kutulisha hivyo tulienda kuishi kwenye nyumba za watu ambao walikuwa wakitutesa. Kutokana na hali hiyo ikawa ngumu kwetu kwenda shuleni,” alisema muimbaji huyo anayeongea taratibu.
Hata hivyo maisha ya Sharon yalibadilika baada ya mama yake kuolewa na mzungu. “Mama yangu aliolewa na mzungu ambaye amekuwa akitulea na kutulipia ada ya chuo.”
Sharon ambaye ana imani kuwa atashinda zawadi ya shilingi milioni tano za Kenya za TPF,anasema atazitumia fedha hizo kurekodi albam na kuipromote.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents