Habari

Sharti upime CORONA kabla ya kufunga ndoa, Rwanda

Suala la kuwataka wanandoa na wageni wao kupima Covid-19 kwa gharama zao ili kuwaruhusu kufanya sherehe za baada ya kufunga ndoa, linaendelea kuzua mjadala mkali nchini Rwanda.

Wakati huu wa Covid-19, ni wageni 30 tu wanaoruhusiwa kuhudhuria sherehe za harusi kulingana na hatua iliyowekwa na serikali ili kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona nchini humo.

Huku gharama za vipimo vya Covid-19 kwa mtu mmoja ni dolla 50.

Jambo ambalo linawafanya baadhi kuamua kufanya hafla ya kanisani tu pasipo kusherehehekea harusi kwa kuhofia gharama hizo, huku wengine wakiahirisha kabisa harusi zao.Manzi Jules &Solange

Manzi Jules na mkewe Solange ambao wamefunga pingu za maisha katika kanisa la Mtakatifu Bosco mjini Kigali hawakuwa na sherehe zozote baada ya ibada ya ndoa.

Na si kwamba sherehe zimekatazwa,la hasha ni kuambatana na maagizo yaliyopo ya kuzuia maambukizi ya Covid-19. Agizo la serikali linahitaji kwamba kufanya sherehe yoyote ya harusi, wanandoa na wageni wao lazima wawe na uthibitisho kuwa walipima Covid-19 na hawana virusi hivyo.

‘’Tuliamua kuja kanisani kupata baraka za Mwenyezimungu tu,haingewezekana kupima waalikwa wote 30,ingenigharimu franga milioni moja unusu($ 1500) tutafanya sherehe muda utakaporuhusu,’’Manzi Jules alisema.

Manzi Jules &Solange

Aidha hatua hiyo ya kupima covid 19 imewalazimu wengine kuhairisha kufunga ndoa.

‘’Masharti haya yalitolewa siku chache kabla ya harusi yangu .niliamua kuahirisha harusi na sherehe zake kwani unajua siku ya harusi hutokea mara moja katika maisha ya mtu .tunaomba serikali kuturahisishia kwa kupima watu kama ilivyofanya tangu mwanzoni mwa Covid-19 au kupunguza gharama ya vipimo’’

Waziri wa mambo ya ndani Anastase Shyaka amesema serikali iliweka masharti hayo ili kuokoa maisha ya wananchi.

Awali Mashirika yasiyo ya kiserikali yaliiandikia serikali kulalamikia hatua zinazochukuliwa zikiwemo hizi za kuwataka watu kugharamia wenyewe vipimo vya covid19 kutokana na hali ya maisha kuzidi kuwa ngumu kwa wananchi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents