SHEAR ILLUSIONS, MUSTAFA HASSANALI WAJITOSA MISS DAR INTER COLLEGE 2012

WAKATI shindano la kumsaka Miss Dar Intercollege 2012
likitarajiwa kufanyika Juni 22 kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa , uliopo
mkabala na chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) duka la vipodozi la Shear
Illusions,pamoja na mbunifu maarufu wa mavazi,Mustafa Hassanali wamejitosa
kudhamini shindano hilo .Awali shindano hilo lilipangwa kufanyika juni 8
kabla ya kusogezwa mbele kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya
warembo kuwa katika mitihani pamoja na mafunzo yao kwa vitendo
ŒField¹.Mratibu wa Shindano hilo Dina Ismail alimesema kwamba Shear lenye
matawi yake jengo la Millennium Tower na Mlimani City linajihusha na uuzaji
wa vipodozi halisi Œoriginal¹ kutoka nje ya nchi litatoa vipodozi kwa
warembo watakaoshiriki,huku Hassanali atatoa zawadi ya magauni ya
warembo.Alisema maandalizi kwa ajili ya shindano hilo yanaendelea ambapo leo
warembo hao ambao awali walikuwa wakifanya mazoezi kwenye hoteli ya Lamada,
jana walihamishia kambi yao kwenye hoteli ya Grand Villa iliyopo Kijitonyama
jijini Dar es Salaam.Dina ameongeza kuwa mpaka sasa wameshapatikana warembo
13 ambao wapo chini ya ukufunzi wa Marylidya Boniface, huku kwa upande wa
shoo wakinolewa na dansa aliyepata kufanya vema miaka ya nyuma, Bob
Rich.³Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss
Dar Intercollege anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania ,²alisema
Dina.Warembo watakaoshiriki shindano hilo wanatoka vyuo vya Biashara (CBE),
Uandishi wa Habari (DSJ) na Time, Ustawi wa Jamii, Usimamizi wa Fedha (IFM)
na Chuo Kikuu huria (OUT ambapo taji linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM,
huku mshindi wa pili wa mwaka jana, Blessing Ngowi alitinga fainali za Miss
Tanzania.Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Veronica Ngota, Rose
Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael,
Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada
Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.Shindano hilo limedhaminiwa na
kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd¹s,Dodoma Wine, Ndege
Insurance, Skylight Band,Lamada Hotel, Screen Masters,Makumbusho ya Taifa,
Mustafa Hassanali, Grand Villa Hotel, Clouds Fm na blog za Michuzi,
Mamapipiro, Bin Zubeiry,Mtaa kwa Mtaa na Fullshangwe

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents