Burudani

Shebby Love kutafuta wasanii atakaowasimamia kupitia studio yake mpya

Msanii Shebby Love, amepanga kutafuta wasanii wenye vibaji ambao atakuwa anawasimamia kupitia studio yake mpya, ambayo anatarajia kuifungua hivi karibuni.

Akiongea na mtangazaji wa kipindi cha Mega Mix cha Abood FM, Simple Bway, Shebby amesema amepanga kutafuta wasanii wenye vipaji kwa kuanzia katika mkoa wa Morogoro ambao atakuwa anasimamia kazi zao.

“Hivi karibuni nafikiria tunaweza kuandaa tour zetu, kuanzia Kilosa, tutakuja Kibira mpaka Mikumi kwa ajili ya kuwatembelea mashabiki zangu pamoja na kutafuta vipaji viwili vitatu vya kuweza kukaa lebo katika studio yangu. Haijalishi nitapata wasanii wa Hip Hop, Singeli, nitabata RnB, Mchiriku hilo halijalishi ilimradi nipate msanii wa kuja kukaa lebo katika studio yangu na kurekodi kazi bure,” amesema muimbaji huyo.

Hitmaker huyo wa Utamu, ameongeza kuwa, akimaliza kutafuta vipaji anavyovitaka katika mkoa huo wa Morogoro ataenda kufanya hivyo tena katika mkoa wa Tanga.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents