Burudani

Sheddy Clever atayarisha wimbo wa Tiwa Savage na KCEE (Video)

Producer wa hit single ya Diamond Platnumz, Number One, Sheddy Clever ametayarisha nyimbo za wasanii wakubwa wa Nigeria, Tiwa Savage na KCEE.

Sheddy ambaye ana studio yake iitwayo Burn Records, ameiambia Bongo5 kuwa fursa ya kutayarisha nyimbo za wasanii hiyo imepatikana kutokana na connection aliyofanyiwa na Diamond. “Tayari nimeshafanya kazi na Tiwa Savage na kuna kazi ambayo nimefanya na KCEE na kuwa wasanii wengine wa South Africa,” amesema Sheddy ambaye alitajwa kuwania kipengele cha mtayarishaji bora wa muziki wa Afrika kwenye tuzo za AFRIMMA 2014.

“Zote ni connection za Diamond, yeye (Tiwa Savage) anafahamiana naye na mimi nilimwambia Diamond ‘nahitaji kufanya naye kazi’ Diamond akaniambia ‘Yeah it’s okay, fanya beat’ akaniunganisha naye, nikawa nachat naye, nikamtumia beat akapenda, tukawa tunafanya kazi online, na ana ngoma pia amefanya na Diamond.”

“Amesharekodi tayari kila kitu na wimbo upo, kwahiyo sasa ni yeye tu sijui atatoa lini ila mimi nahitaji project hizo mwakani ntaomba ruhusa kutoka kwao ili niziachie hapa nyumbani,” aliongeza Sheddy.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents