Siasa

Sheikh Yahya: Mimi si mshirikina

Sheikh Yahya siyo mshirikina

 

Mnajimu mashuhuri wa Afrika Mashariki Sheikh Yahya Hussein, amekana kushirikisha masuala ya uchawi katika utabiri wake na kubainisha kuwa utabiri anaoufanya juu siasa za Tanzania anaufanya kwa watu anaowafahamu pekee.

Akizungumzia utabiri wake juu ya mgombea Uraisi kupitia chama cha mapinduzi Raisi Jakaya Kikwete ambapo hivi majuzi alitamka kumlinda mgombea huyo kutokana na kuanguka kwake katika majukwaa, Yahya amesema amemtabiria ulinzi Kikwete kwa sababu anamfahamu na kwamba hawatambui vizuri wagombea wengine.

Hatua hiyo iliyozua gumzo suala lililokifanya Chama Cha Mapinduzi kukana uhusiano wowote na mtabiri huyo, limemfanya Sheikh Yahya kutoa ufafanuzi juu ya kauli zake huku akisisitiza kuwa hajihusishi na masuala ya kishirikina.

“Mimi si mchawi na sijui uchawi” amefafanua Sheikh Yahya.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents