Tupo Nawe

Shela la Priyanka Chopra kwenye harusi yake na Nick Jonas lazua gumzo, lina urefu wa futi 75

Baada ya kupita kwa harusi ya mwigizaji mashuhuri nchini India, Priyanka Chopra na Mwanamuziki wa Kimarekani, Nick Jonas siku chache hatimaye mwana dada huyo anagonga tena vichwa vya habari hasa kutokana na shela aliloonekana nalo katika ndoyake.

Bollywood actress Priyanka Chopra (L) and US musician Nick Jonas

Shela hilo ambalo limebuniwa na kampuni ya Ralph Lauren, lilikuwa na puleki za lulumizi milioni mbili, zikiwa zimeshonelewa kwa ustadi mkubwa.

Wakati likiwa na urefu wa futi 75,  ambazo ni sawa na mita 23. Shela hiyo ilikuwa nyeupe na laini na yenye kupitisha nuru na kumuwezesha anayetazama kuona kilichomo.

Bollywood actress Priyanka Chopra (L) and US musician Nick Jonas

Mapema kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagraam, Priyanka amelifichua vazi hilo na kuliweka wazi baada ya kukosekana kwa picha zake za harusi tangu kuolewa kwake.

Jonas na Chopra ambao wameachana kwa umri kwa mwongo mmoja walichumbiana majira ya joto, baada ya kupita kipindi cha mapenzi tele na kufunga ndoa wikendi katika jimbo la Rajasthan.

Shela hiyo ilikuwa ndefu sana kiasi kwamba ilihitaji kundi la watu kuibeba. Mtandaoni watu hawakuishiwa na maneno.

https://twitter.com/foutted/status/1069982837607198722

 

Baadhi waliifananisha na vitu vingine.

Wengine nao wakadokeza kwamba ilizidi sana shela ya Meghan Markle, mke wa mwanafalme wa Sussex Harry, ambaye alifunga ndoa miezi kadha iliyopita.

Kitambaa cha shela ya Markle kilikuwa na urefu wa futi 16.

Chopra alivalia vazi hilo la Ralph Lauren katika sherehe iliyoandaliwa katika bustani ya kasri la Umaid Bhawan katika jiji la Jodphur Jumamosi.

 

Sherehe hiyo iliongozwa na babake Jonas, Paul Kevin Jonas, ambaye ni mhubiri.

Sherehe ya harusi yao ambayo ilikuwa ya siku tatu, pia ilijumuisha sherehe ya Kihindi Jumapili ambapo wawili hao walikula kiapo cha uaminifu katika ndoa tena.

Akizungumza na mwandishi wa jarida la People, Chopra alisema kwamba anafurahia kwamba utamaduni ulibadilishwa kuwafaa.

 

Jonas, 26, na Chopra, 36, walichumbiana majira ya joto, si muda mrefu baada ya taarifa za mapenzi yao kuanza kuwa hadharani.

Baadaye walisema kwenye mahojiano kwamba walianza kuwasiliana kwa ujumbe mfupi Septemba 2016.

Walionekana pamoja hadharani katika hafla ya kutoa tuzo za sanaa ya Met Gala Mei 2017 na wote walikuwa wamevalia mavazi ya Ralph Lauren, na uhusiano wao ukaanza kugonga vichwa vya habari mwaka mmoja baadaye.

Chopra ni miongoni mwa wasanii wa Bollywood wanaolipwa pesa nyingi zaidi, na alishinda Miss World mwaka 2000.

Kufikia sasa, ameigiza katika zaidi ya filamu 50 za India.

Alianza kuigiza Marekani katika msururu wa filamu za Quantico na pia katika filamu za Ventilator, Baywatch na A Kid like Jake.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW