Habari

Sheria inayoruhusu mbakaji kumuoa mbakwaji yazua utata

Wanaharakati nchini Lebanon wameandamana kupinga sheria inayomruhusu Mbakaji kuachiwa huru kama ataridhia kumuoa aliyembaka.

Waandamanaji wakiwa wamevalia viboksi kichwani jana jioni Mjini Beirut (Picha na AFP)

Sheria hiyo iliyopitishwa mwaka jana na bunge la nchi hiyo imekosolewa zaidi na wanawake wakidai mswada huo ulipitishwa haraka na kuwa sheria kwa nguvu kumbwa kutoka kwa wabunge wanaume na haikuzigatia maoni ya wanawake ambao ndio waathirika wakubwa.

Maelfu ya watu wakiwemo wanawake mjini Beirut jana waliandamana kushinikiza bunge lijadili upya sheria ya kanuni za adhabu ili kuibadilisha sheria hiyo.

“Hongera kwa wanawake wa Lebanon kwa kupigania haki zenu, ukandamizwaji wa wanawake sio utu hata siku moja naamini hadi hapa tumefanikiwa”,amesema kiongozi wa kundi la ABAAM linaloundwa na wanawake wakiwa kwenye maandano jana jioni.

Taarifa kutoka shirika la utangazaji la AFP zinadai tayari Bunge la nchi hiyo limeunda kamati ya kuangalia namna ya kuibadilisha huku asasi za kiraia na mashirika makubwa ya haki za kibinadamu yakishinikiza sheria hiyo ifutwe na Kamati hiyo leo inatarajiwa kutoa tamko rasmi.

Sheria hiyo inayoruhusu Mbakaji kupunguziwa adhabu kwa kumuoa muathirika inaruhusu pia hata watoto wadogo waliofanyiwa ukatili huo kulelewa na Mbakaji.

Hata hivyo mpaka sasa licha ya sheria hiyo kupitishwa nchini humo hakuna hata kesi moja iliyohukumiwa huku vitendo vya ubakaji vikizidi kushamili.

Juhudi hizo za wanawake zimekuja baada ya wiki mbili zilizopita nchini Jordan kubadilisha sheria ya kanuni za adhabu ambapo sheria kama hiyo ilifutwa.

Pia mwezi wa julai mwaka huu Tunisia ilipitisha sheria mpya zinazowalinda wanawake na watoto dhidi ya vitendo vya ubakaji ili kukomesha vitendo vya kikatili dhidi yao.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents