Mitindo

Sheria Ngowi: Suala kubwa linalowakwamisha watu kwenye interview za kazi ni uvaaji

Mbunifu wa mavazi wa kimataifa kutoka Tanzania, Sheria Ngowi amesema miongoni mwa sababu kubwa zinazochangia kukwamisha watu kwenye usaili wa kazi ni uvaaji.

IMG_9521

Akiongea na Bongo5, Sheria Ngowi amesema uvaaji wa mtu huwasaidia watu wanaofanya usaili kumtambua mtu huyo ni wa aina gani.

“Wewe unaenda kuomba kazi ya udaktari umevaa jeans, tshirt na unavuta sigara, hata yule anayekupa kazi anajua huyu sio daktari mzuri, au unaenda umelewa, anajua kabisa huyu hata kwenye duty ya usiku hawezi akakaa ofisini sababu ni mlevi,” amesema Ngowi.

“Uvaaji unasimama kwa niaba ya wewe, sehemu yeyote. Ndio maana mtu akivaa vizuri hutajua ana hela au hana hela, amekula au hajala, ana matatizo ama hana matatizo. Kwahiyo mtu anapoenda kuomba kazi sehemu ujue hiyo kazi inamhitaji awe vipi, achana na maswali utakayoulizwa, unaweza kwenda interview ukadhani utaulizwa maswali hamsini lakini kwa uvaaji wako ukaulizwa mawili, kwasababu kila kitu anakijua, hana doubt na wewe.”

Msikilize zaidi hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents