Michezo

Shetani alinipitia nikasaini  Simba na Yanga – Buswita

Kiungo wa Yanga SC, Pius Buswita amekiri kusaini mikataba miwili kwenye vilabu viwili tofauti katika msimu mmoja akitokea timu ya Mbao FC ya Mwanza, hatua ambayo imemsababishia rungu la kufungiwa mwaka mmoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Kwa mujibu wa mtandao wa Azam Tv, Buswita ambaye  amesaini Yanga mkataba wa miaka miwili  Ijumaa ya Juni 16, amekiri kufanya kosa hilo kupitia kwa wakala wake, Medi Mtabora huku akieleza sababu kuwa ni kupitiwa na shetani baada ya kubanwa na wahusika waliomsainisha mkataba wa pili.

“Mkataba ninaoutambua ni wa Yanga, nimehusika katika hatua zote kumpeleka Yanga, sasa nashangaa haya yametoka wapi”. Mwenyewe nilipomuuliza amesema shetani alimpitia kwa kuwa hao watu walimbana sana”.Amesema wakala wa mchezaji huyo

Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, ndiyo iliyobaini kuwa mchezaji huyo amesaini mikataba ya klabu mbili tofauti katika msimu mmoja wa 2017/18.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents