Shetta aanzisha kampuni ya kusimamia wasanii, Owkey Music Group

Msanii wa Bonge la Bwana, Shetta ameungana na wasanii wengine wakiwemo AY na Mwana FA kwa kuanzisha kampuni itakayokuwa ikisimamia wasanii hususan wachanga.

shetta1

Akiongea na East Africa Radio leo, Shetta amesema japo bado jina halijawa rasmi, amefikiria kuiita kampuni yake Owkey Music Group na bado yeye na menejimenti nzima wanalijadili jina hilo.

Hata hivyo amesema tayari kampuni yake imeshamchukua msanii mmoja aitwaye Rumi ambaye wimbo wake uitwao Kosa utatambulishwa Jumamosi hii. Ameongeza kuwa baada ya Rumi wapo wasanii watatu watakaosainishwa kwenye kampuni hiyo pia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents