Habari

Shetta adai amepata faida zaidi kuliko hasara baada ya kujitoa ‘Dar Stamina’

Hitmaker wa ‘Sina Imani’, Shetta Bilal, amesema toka kujiondoa katika Kundi la Dar Stamina, muziki unamlipa kutokana na kipato anachokipata kinakidhi kuendesha maisha yake na familia kwa ujumla.

Shetta
Shetta na Menina kwenye Fiesta 2013 Dar

“Ukiwa alone unafanya kuwa maisha yako ya kimuziki hela ya muziki unaiona na vitu kama hivyo. Kwenye kundi sio kama unaiona lakini inakuja taratibu taratibu sana. Kwahiyo mimi kutoka kwenye kundi nikachukua uamuzi sahihi nikaona maisha yanabadilika kwa hiyo ndio faida,”Shetta aliiambia Chumba Cha Sindano kupitia kipindi cha Kali za Bomba, Bomba FM Mbeya.

Akizungumzia sababu iliyomfanya kuandika track ya Sina Imani aliyomshirikisha Rich Mavoko, Shetta alisema ni kwasababu watu walisema anaimba sana mapenzi na hivyo akaamua kuyaimba katika mfumo wa kutoa elimu pia.

“Nilikuwa nimeambiwa naimba sana mapenzi sasa watu walikuwa wanashindwa kuelewa unaweza kumba mapenzi katika kuelimisha na kuburudisha watu wakapata somo na ku-enjoy pia. Nimechokwa wakazungumzia Mdananda, wakazungumzia Nidanganye, Bonge la Bwana. Lakini Sina Imani imekuja ya mapenzi ina ujumbe ndani yake kitofauti kama kucheza kwa sababu ngoma inachezwa Club, inachezwa wapi lakini sometimes ukachill ukisikiliza kwa makini unaelimika.Kwahiyo this time nabadilika badilika kwa sababu mimi nimbunifu toka nilipotoka na chochote mimi nachohisi kwa muda huu kinaweza kuwa ni biashara nakikawa kizuri huwa nakifanyaga.”

Shetta aliongeza kuwa pamoja na kwamba yeye ni rapper, hujitahidi kufanya rap ya biashara zaidi.

“Nikuwa tofauti na watu wanao-rap kwa sababu mimi narap lakini na Rap Commercial, kitu ambacho naweza kurap katika beat ya wasanii wanaoimba. Nimefanya nyimbo nyingi kuna nyimbo mpya ya Abby Skillz kuna niliyofanya na Ali Kiba, ambapo mimi nime-rap, nina nyimbo na msanii kutoka Kenya naye beat hizo hizo za kuimbaimba alikuja tu halafu Manecky akamwambia ‘halo hii beat inatakiwa aimbe Shetta’ na vitu kama hivyo. Kwa hiyo kuna beat hata zikipigwa lazima utasema ‘lazima Shetta afanye’ kutokana na ile style ambayo niliiangalia, nikaicreate. Rap yangu anaweza kusikiliza mtu yeyote awe mtoto wa kike. Haijamlenga kwamba yaani hii ni wagumu tu rap yangu mwanaume, mwanamke, mtoto wote wanapenda that’s why inakuwa hivyo.”

Greyson Chris Bee”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents