Shetta aelezea kwanini amemnunulia mwanae gari la shilingi milioni 12


Wakati mwanae akikaribia kutimiza siku 40 tangu azaliwe, rapper Shetta amezungumza kuhusu sababu za kumnunulia gari aina ya Toyota Opa lenye thamani ya shilingi milioni 12.

“Kitu ambacho nimeamua ni kumpatia zawadi kubwa kama lilivyokuwa jina lake, ye anaitwa Qaylah, Qaylah maana yake ni kitu kikubwa na kizuri kwa hiyo anadeserve. Ni kitu ambacho nilikuwa nakitegemea kwa muda mrefu so for real nimeamua kumpatia hiyo zawadi yake. Ikishakuwa mali yake ni mali yake tu. Najua tumezoea ya kwamba mtu akifikisha miaka 18 ndio anaweza kumiliki kitu fulani au kukitumia sio kukimliki, anamiliki mtu mwenye age yoyote. Kwahiyo hiyo ni mali yake ipo chini ya uangalizi wa mama yake na mimi pia,” Shetta aliiambia 255 ya Clouds FM jana.

Hili ndilo gari alilomnunulia mwanae

“Ni kwaajili yake kutokana na mtoto unajua, kliniki, shopping za hapa na pale na vitu kama hivyo, kwahiyo anatumia.”

Amesema hata kama gari hilo atakuja kuliuza, atahakikisha mwanae akikua atakuta zawadi yake ya gari iko pale pale.

Je! Unadhani gari ni zawadi sahihi kwa mtoto mchanga?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents