Burudani

Shetta akanusha kubebwa kwenye kolabo anazofanya

Hitmaker wa Shikorobo, Shetta amekanusha kubebwa na wasanii anaofanya nao kolabo na kwamba nyimbo anazofanya mwenyewe hazifanyi vizuri.

11352172_1117933304902432_1891157799_n

Shetta ameiambia Bongo5 kuwa nyimbo zake nyingi alizowashirikisha wasanii wengine yeye ndio amekuwa akifanya kazi kubwa.

“Mimi naamini ngoma kama Shikorobo nimeimba chorus mwenyewe na verse mbili mwenyewe,” amesema. “Ningekuwa nimemtoa pia ningefanya vizuri. Kcee amekuwepo kwa sababu ni international artist ili kufanya kubwa zaidi Nigeria, pia yeye anakuhitaji huku na mimi nakuhitaji kule. Kwahiyo amenitumia mimi na mimi nimemtumia yeye.”

“Maneno kama hayo hayaniumizagi as long as nafanya kazi nzuri na ngoma zangu nyingi kazi kubwa nafanya mimi,” amesisitiza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents