Burudani

Shetta ataja anapopata fedha za kula bata mjini

Msanii wa Bongo Flava, Shetta ametaja sehemu anapopata fedha za kuendesha maisha yake hasa katika kipindi alichokuwa kimya kimuziki.

Shetta ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Wale wale’, amesema yeye hana fedha nyingi kama watu wanavyodhani na kiasi alichonancho kinatosheleza maisha yake tu.

“Mimi ni chawa kwa matajiri nikiwa na shida namcheki boss Mo, au matajiri ambao nimetengeneza ukaribu nao na mwisho wa siku mambo yangu yanaenda,” Shetta ameiambia Planet Bongo ya EA Radio.

Msanii huyo ameenda mbali zaidi kwa kusema si kweli kuwa fedha zake anazipata kutokana na biashara ya dawa za kulevya, na kueleza kuwa angekuwa anafanya hivyo nae angetajwa katika orodha ya watuhumiwa wa biashara hiyo haramu.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents