Shetta kumwaga mamilioni kwa wasiojiweza

Ikiwa ni siku 10 kabla ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kuanza, mkali wa Shikorobo, Shetta ametangaza kutoa misaada kwa watu wasiojiweza Tanzania nzima.

Shetta

Muimbaji huyo ambaye yupo kimya kwenye muziki, amedai atatoa kile kidogo alichonacho kwenye vituo mbalimbali vya watoto yatima.

“Msimu wa Ramadhan unakaribia mimi kama Shetta na menejimenti yangu nzima napenda kukufahamisha kuwa kwa kidogo nilichonacho natarajia kuanza kusaidia na kutoa misaada kwa vituo vya watoto yatima na wenye uhitaji mkubwa mikoa yote ya Tanzania ambayo ntaweza kuifikia,” alisema Shetta kupitia taarifa aliyoitoa kupitia mtandao wa Instagram.

Aliongeza, “Naamini vipo vituo vingi vyenye uhitaji mkubwa sana wa mahitaji ya kila siku. Hivyo basi popote ulipo kama unajua au unahusika na kituo chochote usisite kuwasiliana nasi kupitia social media (Instagram, Twitter, FaceBook; @OfficialShetta or @MxCarter) Email; [email protected] or [email protected] Simu; +255 22 278 0288 / 0655653030 Ili tuweze kukufikia kwa urahisi kabisa,”

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW