Soka saa 24!

Shilole awachana wasanii ambao hawamuungi mkono Rais Magufuli, amtumia maombi mazito ‘aniruhusu niuze chakula kwenye Treni’

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Shilole amewachana wasanii wa Bongo Fleva ambao hawamuungi mkono Mhe. Rais John Magufuli huku akimtumia maombi ya kutaka kuuza chakula kwenye Treni mpya za kisasa pindi mradi huo utakapokamilika.

Image result for Rais Magufuli na shilole
Rais Magufuli I Shilole

Shilole akiongea mapema leo kwenye tukio la wasanii kutembelea mradi wa SGR, amesema kuwa wasanii wawe kitu kimoja kwa kumsapoti Rais Magufuli kwa vitu anavyovifanya.

Unajua unavyojichanganya na wenzio ndio unavyopata connections. Mtu ambaye anaitwa na kiongozi wako halafu hautii, hiyo sio heshima, it means huwezi kuheshimu wazazi wako. Unajua unavyoitwa na Rais huwezi jua anakuitia nini?je, akikuteua kuwa mkuu wa mkoa, au mkuu wa Wilaya utakataa?,”amefunguka Shilole na kumuomba jambo Rais Magufuli.

Kwanza nataka nimuombe ombi Mhe. Rais Magufuli, nataka aniruhusu niuze chakula kwenye Treni itakapoanza kazi, mimi sitaki hela nataka tu anipe nafasi hiyo basi

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW