Mapenzi

Shilole kufunga ndoa ya maajabu

Haitakuwa hadithi tena kusikia wapendanao wakifunga ndoa kwenye ndege hususani hapa Tanzania kwani msanii wa bongo fleva, Shilole, yupo mbioni kufanya hivyo na kuweka rekodi mpya ambayo haijawahi kutokea nchini kama sio barani Afrika.

Image result for shilole
                Msanii wa Bongo Fleva,Shilole.

Shilole amesema lengo lake sio tuu kuweka rekodi au kuonyesha ana uwezo mkubwa kifedha la hashaa!! Lengo lake ni kutaka kila shabiki yake kuhudhuria kwenye tukio hilo la kihistoria ambalo litafanyika angani kabla ya helkopita kutua uwanja wa mpira wa Taifa ambako mashabiki wake watakutana kushuhudia harusi hiyo.

Ndoa yangu nitafungia juu ya Ndege (Helkopita),Tukishuka nashukia uwanja wa taifa…,hivi unategemea mimi nitaolewa tuu halafu watu waone picha zangu tuu? Mimi nataka watu waje kushuhudia.Ujue mimi nina mashabiki wengi na wote nataka waje waone Dada Mwajuma aking’olewa“Alisema Shilole kwenye mahojiano yake na Clouds Fm.

Shilole ambae hakutaka kuweka wazi jina la mchumba wake huyo mpya ambae watafunga nae ndoa kwa kuhofia kuporwa na walimwengu alisema mipango ya ndoa ipo ingawaje bado kwanza kuna vitu havijakaa sawa na ikifika muda atawatangazia mashabiki wake.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents