Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Shinda bia kwenye vituo vya Daladala/Mabasi kupitia promosheni ya vuta pumzi kila J’GWARA na safari ndogo (Video+Picha)

Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) kupitia kinywaji chake cha Safari Lager imetangaza rasmi kuwa kuanzia leo Jumatano Machi 21, 2018 itakuwa na promosheni ya VUTA PUMZI KILA J’GWARA NA SAFARI NDOGO ambapo watumiaji wa bia ya safari lager watajishindia kinywaji hicho kwenye vituo vya daladala.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Meneja wa Kampuni hiyo, Kabula Nshimo amesema kuwa promosheni hiyo itahusisha watu walio juu ya miaka 18 na itakuwa siku ya jumatano pekee.

Mtumiaji wa bia hiyo atakwenda kwenye vituo vya Daladala/Mabasi vyenye huduma hiyo ambayo kwa kuanzia Safari Lager wameanza na kituo cha Morocco na baadaye itasambaa vituo vingine vya daladala ndani ya jiji la Dar es salaam.

Kumbuka mashine hizo zitatoa bia kwa siku ya Jumatano pekee kuanzia saaz 10 jioni hadi saa 6 usiku na washindi wote watapelekwa kwenye Bar zilizokaribu na kituo husika msikilize hapa chini Bi. Nshimo.

Tazama baadhi ya picha hapa chini kuona baadhi ya watu waliohudhuria kwenye uzinduzi huo wa kituo hicho kidogo cha Morocco jijini Dar es salaam.

 

 

 

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW