Habari

Shirika la Ndege la Kenya latangaza hasara zaidi

Shirika la taifa la safari za ndege nchini Kenya, Kenya Airways(KQ) limetangaza kupata hasara ya kifedha mwaka uliopita kwa takriban dola za Kimarekani milioni 75.

Ndege ya kampuni ya Kenya Airways

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Hasara hiyo ambayo ni sawa na shilingi za Kenya 7.59 ilirekodiwa katika kipindi cha miezi 12 hadi mwishoni mwa mwaka 2018.

Hata hivyo kiwango hiko cha hasara ni kidogo kuliko cha mwaka jana ambayo ilikuwa ni shilingi bilioni 9.44 katika kipindi cha mwaka 2017.

Taarifa hii imechapishwa katika ukurasa wa jarida maarufu la maswala ya uchumi na fedha:

Kampuni hiyo inasema kwa hasara imetokana na ongezeko kubwa la bei ya mafuta, mishahara ya juu, na viwango vya juu vya gharama za usafiri wa ndege vilivyowekwa na mmiliki.

Hata hivyo kulikuwa na ongezeko la mapato ya kiasi cha Shilingi bilioni 114.45 ikilinganishwa na mwaka jana ambapo yalikuwa ni Shilingi bilion 106.2. Mapato hayo ni ya chini ukilinganisha na kiasi cha Shilingi 116 bilioni yaliyopatikana mwaka 2016.

Shirika hilo la ndege la kimataifa limekuwa likitumia suala la hasara linayoipata kujaribu kuchukua utawala wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta, lakini Wakenya wengi wamekuwa wakielezea kutokubaliana na hoja hiyo.

Ni zipi sababu za harasa inayoipata Kenya Arways?

Kulingana na tume ripoti ya tume ya seneti iliyochukua jukumu la kuelewa mzozo wa hasara katika Kenya Airways mwaka 2015, iliyoongozwa na Seneta Anyang’ Nyong’o, sababu tano zilibainishwa, lakini wachanganuzi wa masuala ya uchumi wanasema hakuna aliyejali kuzitafutia suluhu.

Sababu tano zilizotajwa kusababisha hasara katika KQ:

Baadhi ya Wakenya wamekuwa wakielezea hisia zao juu ya hasara inayoendela kulikumba shirika la ndege la taifa lao kenya Airways.

Mfano picha hii ya kibonzo iliyotumwa kwenye mtandao wa kijamii inaelezea kwa kifupi hisia za baadhi ya wakenya juu ya tangazo la hasara kwa KQA :

https://twitter.com/Dennismaina4/status/1123112631735398400

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents