Habari

Shirika la Posta lawatumbua vigogo wanne

Bodi ya Wakurugenzi Shirika la Posta Tanzania, imetengua nafasi tatu za mameneja na ofisa mwandamizi kutokana na vitendo vya urasimu, kufanya kazi kwa mazoea, ubadhilifu na wizi.

Mameneja waliotenguliwa ni James Sando ambaye alikuwa Meneja Mkuu, Menejimenti ya Rasilimali. Macrice Mbodo ameteuliwa kushika nafasi hiyo, Meneja Mkuu Uendeshaji wa Biashara Janeth Msofe, aliyekuwa Meneja wa Mkoa Shinyanga huku Hassan Mwang’ombe akiteuliwa kushika nafasi hiyo.

Aidha bodi hiyo pia imewasimamisha kazi Meneja Msaidizi wa Barua na Logistic, Jasson Kalile na Ofisa Mwandamizi wa Usafirishaji, Ambrose John.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya shirika hilo, Haruni Kondo, ameyasema hayo wakati akizungumza na wanahabari kuwajulisha uamuzi uliofanywa na bodi.

“Imebainika na imewaridhisha kuwa baadhi ya watendaji wakuu wa makao makuu ya Posta wamekuwa kikwazo katika dhana ya uwajibikaji, weledi na kujituma katika kutekeleza wajibu na majukumu yao, ili kulifanya shirika hilo kuwa mfano bora wa mashirika yenye ubora katika kutoa huduma,” alisema Dk Kondo huku akitolea mfano wa mkataba wenye utata wa kukodisha magari ya kusafirisha barua kuwa kukodisha magari kwa siku inalipwa shilingi milioni 10, kwa wiki shilingi milioni 70 na kwa mwezi shilingi milioni 300.

By: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents