Tupo Nawe

Shirikisho la Soka Duniani Fifa limesitisha mpango wa kuongeza nchi zitakazoshiriki Kombe la Dunia mwaka 2022, latoa sababu hizi

Shirikisho la Soka Duniani Fifa limesitisha mpango wa kuongeza nchi zitakazoshiriki Kombe la Dunia mwaka 2022, latoa sababu hizi

Shirikisho la Soka Duniani Fifa limesitisha mpango wa kuongeza nchi zitakazoshiriki Kombe la Dunia mwaka 2022 hadi timu 48. Rais wa Fifa Gianni Infantino mwaka jana alisema mpango wa kuongeza timu hizo kutoka 32 ambao ungelianza kutekelezwa mwaka 2026 urudishwe nyuma hadi mwaka 2022. Mabadiliko hayo yalimaanisha Qatar ambayo ndio mwandalizi wa mashindano hayo kushirikiana na mataifa mengine katika kanda hiyo.

Kwa mujibu wa BBC.Shirikisho hilo lilisema “baada ya mashauriano ya kina” tumeonelea mabadiliko hayo “hayawezi kutekelezwa kama ilivyopangwa awali”.

Fifa mia imesema ilitathmini uwezewkano wa Qatar kuandaa peke yake mashindano hayo ikiwa na timu 48 lakini ikaamua kusitisha mpango huo kutokana na changamoto ya ukosefu wa muda wa kutosha wa “kufanya ukaguzi wa kubaini athari ya hatua hiyo, matokeo yake na jinsi ya kushughulikia masuala ibuka “.

Taarifa ya waandalizi wa Kombe la Dunia nchini Qatar ilisema: “Qatar ilikuwa tayari kutekeleza mpango huo katika mashindano ya mwaka 2022 na hatua iliyokua imefikia kufanikisha mpango huo ilikuwa umeafikiwa na na wadaou wote.

Gianni InfantinoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRais wa Fifa Gianni Infantino anataka mataifa 48 yashiriki

Infantino, 46, ambaye alimrithi raia mwenzake Sepp Blatter kama rais wa Fifa mwezi Februari 2016 alifanya kampeni akiahidi kupanua michuano hiyo.

Awali alipendekeza michuano ya timu 40, wazo lililowasilishwa na rais wa wakati huo wa Uefa Michel Platini 2013, kabla ya kubadilisha msimamo na kuunga mkono michuano ya timu 48.

“Huku zikiwa zimesalia miaka mitatu na nusu kuelekea mashindano hayo, Qatar imejitolea kuhakikisha inaandaa Kombe la Dunia la mwaka 2022 ambalo litaifanya eneo zima la Uarabuni kujivunia.”

Mwezi Novemba, rais wa Uefa Aleksander Ceferin alisema kuongeza timu 16 katika mashindano hayo ya Qatar 2022 huenda “ingelileta matatizo” na kuongeza kuwa mpango huo”hauwezekani”.

Wale waliyo karibu na waandalizi wa mashindano hayo ya Qatar 2022 wanasema uamuzi wa pamoja ulikua umefikiwa kati yao na Fifa, lakini sasa wameamua kuangazia timu 32 zitakazoshiriki.

Uamuzi huo wa Fifa hatahivyo umewapunguzia waandalizi hao tumbo joto la kushirikiana na mataifa mengine kuandaa mashindano hayo maarufu duniani ikizingatia uhasama uliyopo kati ya taifa hilo na majirani zake.

Saudi Arabia, Milki ya nchi za Kiarabu na Baharain zimeiwekea vikwazo Qatar, na hatua ya kushirikiana nao kuandaa mashindano hayo ingelikumbwa na utata.

Mzozo kati ya mataifa hayo uliiacha Qatar na uwezo wa pengine kushirikiana na Kuwait na Oman lakini utafiti wa Fifa ulibaini kuwa mataifa hayana uwezo wa kufikia masharti yake.

Infantino aliwahi kushauriana na Saudi Arabia wakati alipotoa pendekezo la kuboresha mashindano ya Kombe la Dunia, na wengi walishuku huenda tamko lake kwamba taifa hilo linaweza kuwa sehemu ya suluhisho la kufikia mpango wa kupanua mashindano hayo mwaka 2022.

Lakini kufuatia tuhuma za mwaka jana za mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi katika ubalozi wake mdogo mjini Istanbul, pamoja na jukumu lake katika mzozo wa Yemen huenda Fifa ingelikosolewa na watetezi wa haki za kibinadamu laiti wangelipewa idhini ya kushirikiana na Qatar kuaandaa kwa pamoja mashindano hayo sawia na kama UAE wangelipewa nafasi hiyo kwasababu ni mshirika wake mkuu.

Baadhi ya mashirikisho mengine ya soka ya kitaifa pamoja na Infantino huenda wakasikitishwa na uamuzi huo lakini wengine wengi wanaunga mkono hatua hiyo.

Historia ya Mabadiliko Kombe la Dunia

Kombe la DuniaTimu
1930 Uruguay13
1934 Italia16
1950 Brazil13
1954 Uswizi16
1958 Sweden16
1974 Ujerumani Magharibi16
1982 Uhispania24
1986 Mexico24
1998 Ufaransa32
By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW