Burudani

‘Show Me’ ya Harmonize na Rich Mavoko ni ‘copy & paste’ ya Emergency?

‘Show Me’ ya Harmonize na Rich Mavoko ni moja kati ya ngoma kali za kudance zinazofanya vizuri sehemu mbalimbali ikiwemo kwenye klabu za usiku. Wimbo huo umetayarishwa na Lizer kutoka studio za WCB huku video yake ikiongozwa na director Nicorux kutoka South Afrika.

Lakini wimbo huo umekuwa ukizua mijadala katika mitandao ya kijamii kwa madai wimbo huo ulikuwa ni idea ya wimbo ‘Emergency’ wa msanii wa Nigeria, Sold Star.

Hizi ni baadhi ya rekodi zinazohusu nyimbo hizo mbili.

Harmonize na Rich Mavoko wameachia wimbo wao huo kwenye mtandao wa YouTube April 16 mwaka 2017 na tayari umeshatazamwa mara 2,381,050 kupitia mtandao huo.

Na wakati huo huo video ya wimbo ‘Emergency’ imeachiwa Novemba 24 ya mwaka 2016 katika mtandao wa YouTube. Mdundo wa wimbo huo na baadhi ya melody zake unafanana na ‘Show Me’ wa Harmonize na Rich Mavoko.

Wimbo huo wa Sold Star unatakriban miezi saba tangu ulipoachiwa kwenye mtandao huo umefanikiwa kutazamwa mara 252,433.

Wimbo huo pia unapatikana katika albamu mpya ya msanii huyo W.E.E.D ambayo pia imewashirikisha mastaa kibao akiwemo 2Face, Timaya, Davido, Patoranking, Phyno, Harrysong, Flavour, Tiwa Savage, Burna Boy na Diamond Platnumz kwenye wimbo wa ‘Money’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents