AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Show mpya ya Salama Jabir ‘Ngaz Kwa Ngaz’ kuanza kuruka leo EATV

Kipindi kipya cha runinga cha Salama Jabir kiitwacho Ngaz Kwa Ngaz kitaanza kuruka leo saa tatu usiku kupitia East Africa TV.

Kipindi hicho kinakuja kama mbadala wa kipindi kilichoshinda tuzo cha Mkasi ambacho kilimweka Salama kuwa mmoja wa watangazaji wa TV wanaopendwa Tanzania.

Japo hakuna maelezo rasmi ya jinsi kipindi hicho kitakavyokuwa, promo zake zinaonesha kuwa kutakuwa kunachezwa video mbalimbali za muziki.

Kipindi hicho kinatayarishwa na kampuni ya Mkasi TV iliyoanzishwa na Salama, AY na Josh Murunga.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW