Show ya Mwana FA kwenye Fiesta yageuka gumzo kwenye mitandao ya kijamii, haijawahi kutokea!!

Kwa kujiamini kabisa, tunasema haijawahi katika historia ya Fiesta na show za muziki wa Tanzania msanii kusifiwa kwa kazi nzuri aliyoifanya kwenye stage kama ilivyokuwa kwa Mwana FA! Huenda sababu ikawa ni kukua kwa mitandao ya jamii kama Twitter ambapo mashabiki wana nafasi rahisi kutoa pongezi zao kwa msanii husika lakini seriously Mwana FA aka Binamu aliangusha performance kali pengine kuliko zote alizowahi kuzifanya kiasi cha jana kwenye Twitter kugeuka mjadala na hata kuifunika show ya Rick Ross ambayo nayo ilikuwa kali sana.

Mwana FA aliingia stejini kwa plan nzuri ya namna ya kuimba nyimbo zake. Tunahisi alifanya rehearsal na maandalizi ya maana. Akiwa na T-shirt nyekundu yenye maandishi ‘CAN’T STOP THE HUSTLE & GRIND na miwani iliyokuwa na mishikio yenye rangi nyekundu pia, alionekana smart kinoma.

FA alikuwa ameandaa nyimbo zaidi ya sita zilizohit kinoma na kuchagua kuziimba verse moja moja huku kila moja ikishangiliwa na mashabiki. Kwa kujiamini, FA aliyekuwa mcheshi muda wote aliweza kuongea na mashabiki kuliko msanii yoyote aliyepanda siku hiyo isipokuwa Rozay tu.

‘Zipo nyingi, sasa ntafanyeje?’ alisikika FA mara nyingi baada ya kuwa anakatisha nyimbo zake ili kuimba nyingine. Unanitega, Mabinti, Binamu, Yalaiti, Habari Ndio Hiyo, Unajinua Unasikia, Naongea na wewe na zingine ziliamsha shangwe za wengi kwenye viwanja vya Leaders.

Akiongea leo kwenye kipindi cha Power Breakfast kutoa shukrani kwa wananchi kwa jinsi walivyoiunga mkono Fiesta, mkurugenzi mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kussaga, amesema wapo wamarekani waliomfuata na kumuuliza ‘who is that guy’ wakati FA alipokuwa kwenye stage.

Kwa namna yoyote ile, performance hiyo ya aina yake ya rapper huyo ambaye jina lake halisi ni Hamis Mwinjuma, imefungua ukurasa mwingine mpya wa heshima aliyonayo ndani na nje ya nchi na huenda ikampa michongo mingi zaidi. Kiukweli FA, amelitumia vema jukwaa la Fiesta na huo ndio tunauita ‘ukomavu’.

Hizi ni baadhi ya tweets zilizokuwa zikisifia show ya Mwana FA.







Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents